| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Degedege. Kukosa pumzi. Kupoteza fahamu. Kifo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa matibabu. Tazama Vidokezo.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
|
| Macho |
MWUKE UTAFYONZWA! Wekundu. (Ona Kuvuta pumzi).
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Usitoe msaada wa kupumua kwa kupuliza mdomo kwa mdomo. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari haraka. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
|
Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: F+, T+, N R: 12-26-50/53 S: (1/2-)-7/9-16-36/37-38-45-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Jasara tanzu za UN: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: I | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1051 Msimbo wa NFPA: H 4; F 4; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Baridi. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI AU KIOEVU CHENYE HARUFU TAMBULISHI. ISO RANGI HATARI KWA MWILI: Gesi hii huchanganyika vema na hewa, mchanganyiko unaolipuka hutokea kwa urahisi. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kukanza, kwa kuathiriwa na besi, zaidi ya 2% ya maji, au iwapo haijabadilishwa na kemikali, kwa athari ya moto au mlipuko. Inapowaka hutengeneza gesi babuzi na zenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji, kloridi hidrojeni katika mmumunyo wa alkoholi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 4.7 ppm; (Kiwango cha juu); (ngozi); (ACGIH 2003). MAK: 1.9 ppm, 2.1 mg/m³; H; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2002). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Mchanganyiko unaoweza kudhuru yaweza kutokea kama dutu hii inavukiza kwa hewa yenye joto ya 20°C kufikiwa kwa haraka sana. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ubadilishaji hewa wa seli kusababisha degedege na kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri tezi thioridi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 26°C Kiwango myeyuko: -13°C Uzito wiani (maji = 1): 0.69 (kioevu) Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 82.6 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.94 |
Kiwango cha kumweka: -18°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 538°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.6-40.0 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.25 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu Sianidi ya haidrojeni, iliyoimarishwa, ikafyonzwa katika kitu kinachoweza kunyonya maji kilichotulia. Namba nyingine za UN: 1613, Sianidi ya haidrojeni, myeyusho wa maji, si zaidi ya 20% ya sianidi ya haidrojeni; 1614 Sianidi ya haidrojeni iliyoimarishwa, ikafyonzwa katika kitu kinachoweza kunyonya maji kilichotulia; 3294 myeyusho wa Sianidi ya haidrojeni katika alkoholi, usiozidi 45% ya siyanidi ya haidrojeni. Usifanye kazi peke yako mahali hapo pana uwezekano wa kuwepo sianidi hidrojeni. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||