| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua mno.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Povu. Poda kavu. Dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa koo. Kutapika. Kupoteza fahamu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
|
Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S2370 Msimbo wa NFPA: H 1; F 3; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji. Baridi. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. HATARI ZA KIKEMIKALI: Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 50 ppm kama TWA; (ACGIH 2004). MAK haijathibitishwa. |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera kwa upole macho na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Mfiduo wa viwango vya juu husababisha kupungua fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 63°C Kiwango myeyuko: -140°C Uzito wiani (maji = 1): 0.7 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.005 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 18.7 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.9 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.4 Kiwango cha kumweka: -26°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 253°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.2-6.9 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.39 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||