2-ETHYLHEXYL ACRYLATE ICSC: 0478
Novemba 2003

Acrylic acid, 2-ethylhexyl ester
Octyl acrylate
2-Propenoic acid, 2-ethylhexyl ester
2-Ethylhexyl 2-propenoate
CAS # 103-11-7 C11H20O2 / CH2=CHCOOC8H17
RTECS # AT0855000 Masi ya molekuli: 184.3
UN #
EC # 607-107-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni, mnyunyizio wa maji laini.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 82°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 82°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vyenye mifuniko. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Vazi linalokinga kemikali.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 37/38-43
S: (2-)-24-37
Angalia: [D]
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 2; F 2; R 2;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka gizani. Hifadhi iwapo tu imetulia.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-ETHYLHEXYL ACRYLATE ICSC: 0478
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke hauzuiliki na unaweza kuwa polima na kufunga tundu.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii kupolimisha haraka kwa kuathiriwa na mwanga, joto na peroksidi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: Sh; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 213.5°C
Kiwango myeyuko: -90°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.89
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 19
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.35
Kiwango cha kumweka: 82°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 252°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-6.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.67
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005