| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 45°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 45°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Udhaifu. Kupoteza fahamu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
|
Ainisho ya EU Alama: T R: 60-61-20/21/22 S: 53-45 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-III Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R ; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, asidi kali. Weka gizani.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, besi kali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 ppm kama TWA; (ngozi); (ACGIH 2003). MAK: 5 ppm, 25 mg/m³; H; Aina ya kiwango cha juu: II(8); Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2003). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Mvuke huu inakera kwa upole macho. Dutu hii huweza kuathiri uboho na mfumo mkuu wa neva. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha vidonda vya seli za damu na kuharibika kwa figo (mfiduo wa viwango vya juu). Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kupoteza fahamu. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri uboho na damu kusababisha vidonda vya seli za damu na kuharibika kwa figo. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 145°C Kiwango myeyuko: -65°C Uzito wiani (maji = 1): 1.01 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.27 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01 Kiwango cha kumweka: 45°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 380°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.5 (93°C) - 12.3 (93°C) Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.121 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama. Madhara ya afya yatokanayo na kuingia mwilini dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Athari za kiafya ni chache ikilinganishwa na dutu za aina hii.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||