ETHYLENE ICSC: 0475
Machi 1996

Ethene
(silinda)
CAS # 74-85-1 C2H4 / CH2=CH2
RTECS # KU5340000 Masi ya molekuli: 28.0
UN # 1962
EC # 601-010-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza). Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kusinzia. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi


Macho


Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Uingizaji hewa. Ondosha vyanzo vya moto na funga gesi kwenye unganisho endapo inawezekana. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Alama: F+
R: 12
S: (2-)-9-16-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 136
Msimbo wa NFPA : H 1; F 4; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYLENE ICSC: 0475
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI ILIYOBANWA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi ni nyepesi kuliko hewa. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huweza kupolimisha kufanyiza misombo aromatiki kutokana kukanza zaidi ya 600°C. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (asfiksianti sahili) (ACGIH 1995-1996)
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Isipodhibitiwa gesi hii huweza kusababisha kukosekana hewa kwa kupunguza kiasi cha oksijeni hewani katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mfiduo huweza kuleta kupungua kwa fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: -104°C
Kiwango myeyuko: -169.2°C
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 15°C: 8100
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.98
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 490°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.7-36.0
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005