| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni. USITUMIE maji.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 38°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 38°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kuchanganyikiwa. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Maumivu.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwani ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kichefuchefu. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Jasara tanzu za UN: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFT1-III
|
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Baridi. Weka katika gesi ajizi. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI NYEPE, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha. Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yanayokereketa. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 ppm (kiwango cha juu); (ACGIH 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ini na mafigo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 148°C Kiwango myeyuko: -80°C Uzito wiani (maji = 1): 0.9 Umumunyifu katika maji: hakuna Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 560 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.1 |
Kiwango cha kumweka: 38°C o.c. | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||