ALUMINIUM PHOSPHIDE ICSC: 0472
Aprili 1997

Aluminum phosphide
CAS # 20859-73-8 AlP
RTECS # BD1400000 Masi ya molekuli: 58
UN # 1397
EC # 015-004-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na asidi na maji.
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine. USITUMIE maji.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na asidi na maji.


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kutapika.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mchomo.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Kuhara. Maumivu ya tumbo. Kuumwa kichwa. Degedege. Mshtuko au kuzimia. Kupoteza fahamu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vinavyokalafatika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, T+, N
R: 15/29-28-32-50
S: (1/2-)-3/9/14-30-36/37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43GWT2-I
Isodhurika kwa moto. Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na asidi, maji, vyakula na malisho. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ALUMINIUM PHOSPHIDE ICSC: 0472
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE KIJIVU ISIYOKOZA AU MANJANO ISIYOKOZA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapogusana na maji, hewa yenye unyevuunyevu na asidi huzalisha gesi zenye sumu au ziwakazo (fosfini ICSC 0694).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. Hidrolisisi ya dutu hii kwa unyevu au kutoa jasho yaweza kuleta hewa isiyosafu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye fosfini kutoka kwa fosfidi alumini kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva na njia ya upumuaji kusababisha kuharibika kwa utendaji na kutoweza kupumua. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: >1000°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.9
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kwa kawaida, ambatani ya kusababisha kutakua na hewa (mazao ya kibiashara) yaweza kuwa ni 57% y kiambato kali. Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Alutal, Celphide, Celphine, Celphos, Delicia Gastoxin, Detia Gas-Ex-B, Detia Gas-Ex-P, Detia Gas-Ex-T, L fume, Phosfume, Phostek, Phostoxin, Quickfos, Zedesa ni majina ya kibiashara. Ona ICSC 0694 Phosphine.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005