ETHANETHIOL ICSC: 0470
Oktoba 2004

Ethyl mercaptan
Thioethyl alcohol
CAS # 75-08-1 C2H5SH
RTECS # KI9625000 Masi ya molekuli: 62.1
UN # 2363
EC # 016-022-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Tetemeko. Udhaifu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn, N
R: 11-20-50/53
S: (2-)-16-25-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S2363
Msimbo wa NFPA: H 2; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHANETHIOL ICSC: 0470
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yenye sumu pamoja na sulfidi hidrojeni oksidi za sulfuri. Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na asidi kali kuzalisha gesi zenye sumu, sulfidi hidrojeni na oksidi za sulfuri.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: 0.5 ppm, 1.3 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kupungua kwa fahamu na matatizo ya kupumua.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 35°C
Kiwango myeyuko: -144.4°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.839
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.68
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 58.9
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.14
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.5
Kiwango cha kumweka: -48.3°C
Jotoridi la kujiwasha: 299°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.8-18.2
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.5
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005