2,4-DINITROPHENOL ICSC: 0464
Machi 1996

1-Hydroxy-2,4-dinitrobenzene
CAS # 51-28-5 C6H4N2O5 / C6H3(OH)(NO2)2
RTECS # SL2800000 Masi ya molekuli: 184.11
UN # 1320 (maji > 15% huongenezwa)
EC # 609-041-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Maji mengi.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko.
USIACHE kikaathiriwa na msuguano au mshtuko.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi (Tazama Kumeza).
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Ukwaru. Kubadilika kuwa njano. (Tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Mpapatiko. Kutokwa jasho. Kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Usiruhusu kukauka. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo. Pangusa salio katika mchanga au maunzi ajizi mengine kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/24/25-33-50
S: (1/2-)-28-37-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.1
Jasara tanzu za UN: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 41GDT-I
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4-DINITROPHENOL ICSC: 0464
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO (tazama Vidokezo).

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Huweza kutengana kwa mlipuko kutokana na mshtuko, msuguano, mtikiso. Huweza kulipuka wakati wa kukanza. Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa alkali, amonia na metali nyingi. Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha gesi zenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri kimetaboliki, kusababisha joto la juu la mwili. Mfiduo huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo wa neva wa pembeni. Dutu hii huweza kuathiri macho kutokuona kunakochelewa kutokea (cataract).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: hujisablimisha
Kiwango myeyuko: 112°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.68
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 54.5°C: 0.14
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.36
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
VIDOKEZO
Tumia njia zote zilizopo kwa kupunguza jotoridi la mwili. Kwa sababu ya maumbile yake yakulipuka msombo hutumika pamoja na maji kama lahamu. UN 0076 hutumika kwa msombo mkavu. CAS 25550-58-7 hutumika kwa mchanganyiko ya isoma ya dinitrofenoli.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005