| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Udhaifu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kupumua kwa shida.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpe tope chujio la mkaa ulioamilishwa katika maji anywe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Shauriana na mtaalam. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T+, N R: 26/27/28-33-50/53 S: (1/2-)-28-36/37-45-60-61 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1597-S au 61GT2-II Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 4; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE NYEUPE HADI MANJANO HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Huweza kulipuka wakati wa kukanza hata bila hewa. Inapowaka hutengeneza mafusho na gesi zenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali, besi kali, na metali vinakisishaji, mfano zinki na bati, kusababisha athari ya moto na mlipuko. Michanganyiko na asidi nitriki ni kilipukaji kikali! VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.15 ppm kama TWA (ngozi) (ACGIH 2004). MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ini kusababisha kuharibika kwa ini. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha anemia. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 319°C Kiwango myeyuko: 118°C Uzito wiani: 1.6 g/cm³ Umumunyifu katika maji: ni dhaifu Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: <0.1 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.8 |
Kiwango cha kumweka: 150°C c.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.69 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Ona ICSC 0725 (Dinitrobenzene, mixed isomers), 0691 (1,3-Dinitrobenzene), 0692 (1,4-Dinitrobenzene).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||