DIMETHYL SULPHOXIDE ICSC: 0459
Oktoba 2000

Methyl sulphoxide
DMSO
CAS # 67-68-5 C2H6OS / (CH3)2SO
RTECS # PV6210000 Masi ya molekuli: 78.1
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 87°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 87°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Kiwaa.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Kusinzia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Special attention to avoid skin absorption. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni).
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA : H 1; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Weka gizani. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIMETHYL SULPHOXIDE ICSC: 0459
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KIRISHAI KISICHO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za sulfuri. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali kama vile paklorati.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo) kuingia kupitia kwa ngozi (H); (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Mfiduo wa viwango vya juu ya dutu hii husababisha kupungua fahamu. Dutu hii yaweza kuongeza uwezo wa ngozi kufyonza ya kemikali nyinginezo (tazama Vidokezo).

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini na damu, kusababisha kuharibika kwa utendaji na vidonda vya seli za damu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 189°C
Kiwango myeyuko: 18.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.1
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 59.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.7
Kiwango cha kumweka: 87°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 215°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.6-42.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -1.35 (imekadiriwa)
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Uangalifu mkubwa unatakiwa endapo DMSO ambayo ina sumu kali ipo; kwa sababu ya kuongezeka kwa uwezo wa ngozi wa kufyonza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005