2,4-XYLENOL ICSC: 0458
Mei 2003

2,4-Dimethylphenol
m-Xylenol
1-Hydroxy-2.4-dimethylbenzene
CAS # 105-67-9 C8H10O / (CH3)2C6H3OH
RTECS # ZE5600000 Masi ya molekuli: 122.17
UN # 2261
EC # 604-006-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kukosa pumzi. Tazama Vidokezo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Mavazi ya kinga. Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kama imo katika hali ya uoevu: kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo plastiki vyenye mifuniko. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 24/25-34-51/53
S: (1/2-)-26-36/37/39-45-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 2; F 1; R ; 0
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-II
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, anhidridi za asidi, kloridi za asidi, besi na vioksidishaji.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2,4-XYLENOL ICSC: 0458
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO HADI KAHAWIA AU FUWELE ISO RANGI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha gesi zenye sumu na mafusho yakerayo. Humenyuka pamoja na anhidridi asidi, kloridi asidi, besi, vioksidishaji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kwa kumeza na kupitia kwenye ngozi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa ngozi njia ya upumuaji. na macho. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya aerosoli kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo).

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 211.5°C
Kiwango myeyuko: 25.4-26°C
Uzito wiani: 0.97 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.79
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 8
Kiwango cha kumweka: >112°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 599°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1-6.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.3
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Kuzidisha kwa kemikali yaweza kutokea kwa samaki.
VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005