| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 58°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 58°C, uingizaji hewa.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Kusikia joto na kujaa usoni.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA!
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: T R: 61-20/21-36 S: 53-45 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S2265 au 30GF1-III Msimbo wa NFPA : H 1; F 2; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, halojeni.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji, nitrati na hidrokaboni halojeni. Hushambulia baadhi ya plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 10 ppm kama TWA; (ngozi); A4; (ACGIH 2004). MAK: 10 ppm, 30 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia kwenye ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho. Dutu hii huweza kuathiri ini, kusababisha manjano ya macho na ngozi. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri .ini, kusababisha kuharibika kwa utendaji. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 153°C Kiwango myeyuko: -61°C Uzito wiani (maji = 1): 0.95 Umumunyifu katika maji: kuchanganyika Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: takribani 492 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00 Kiwango cha kumweka: 58°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 445°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.2-15.2 at 100°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.87 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Dalili hazijitokezi mpaka baada ya masaa hadi siki kadhaa kupita. Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii yamechunguzwa lakini hayajaonekana.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||