DIISOPROPYLAMINE ICSC: 0449
Aprili 1997

DIPA
N-(1-Methylethyl)-2-propanamine
CAS # 108-18-9 C6H15N / CH3CH(CH3)NHCH(CH3)CH3
RTECS # IM4025000 Masi ya molekuli: 101.2
UN # 1158
EC # 612-129-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara. Usigusishe na vioksidishaji.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Maumivu. Malengelenge.
Mavazi ya kinga.
Kwanza suuza kwa maji mengi, halafu vua nguo zilizosibikwa na suuza tena. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwani ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. Mchomo. Kichefuchefu. Mshtuko au kuzimia. Kuumwa koo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: F, C
R: 11-20/22-34
S: (1/2-)-16-26-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GFC-II
Msimbo wa NFPA : H 3; F 3; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali. Baridi. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
DIISOPROPYLAMINE ICSC: 0449
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa, huzalisha mafusho yenye sumu ya oksidi za nitrojeni. Dutu hii ni besi kali humenyuka vikali ikiwa na asidi na husababisha ulikaji hadi shaba, zinki na aloi zake, alumini na galvanized steel. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm kama TWA; (ngozi); (ACGIH 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Inayotoza machozi. Mvuke huu husababisha ulikaji kwa macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mgusano na macho ya mvuke wake au kioevu kusababisha kuona maruweruwe. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 84°C
Kiwango myeyuko: (tazama Vidokezo) -61°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.72
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 9.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.5
Kiwango cha kumweka: -6°C o.c.
Jotoridi la kujiwasha: 316°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.8-7.1
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.64
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Viwango myeyuko vingine: -91°C na -96°C. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005