| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kukosa pumzi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Maumivu. Malengelenge. Zaidi tazama Kumeza.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kutetemeka. Udhaifu. Degedege. Kupumua kwa shida. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 22-24-34-51/53 S: (1/2-)-26-36/37/39-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S2020 Msimbo wa NFPA : H ; F 1; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, vyakula na malisho. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ZISIO NA RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapowaka hutengeneza gesi yenye babuzi (kloridi hidrojeni). Inapokanzwa, hutoa mafusho yenye sumu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Hubabua. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Kuwa katika mazingira yenye kiasi kidogo cha myeyuko au kioevu cha dutu kunaweza kusababisha ngozi kuinyonya kwa wingi na kifo cha ghafla. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 210.0°C Kiwango myeyuko: 45.0°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.5 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 53°C: 133 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.6 |
Kiwango cha kumweka: 114°C o.c. Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.06 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Hakuna data za kutosha kuhusu athari za dutu hii kwa afya ya binadamu, kwa hiyo unahitajika uangalifu mkubwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||