| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki lakini huongeza mwako wa dutu nyingine. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usigusishe na dutu ziwakazo. Usigusishe na vinakisishaji vikali, besi kali, amonia, urea, maji.
|
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Hatari ya moto na mlipuko inapogusana na vinakisishaji vikali, besi kali, amonia, urea, maji.
|
|
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Upofu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Kuumwa koo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vikavu. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usifyonze katika vumbi la mbao au vifyonzi vinginevyo viwakavyo. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: O, Xn, N R: 8-22-31-36/37-50/53 S: (2-)-8-26-41-60-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 5.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 51GO2-I+II+III
|
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, tazama Hatari za Kikemikali. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE NYEUPE, YENYE HARUFU KALI. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa, inapogusana na maji, huzalisha mafusho yenye sumu, kama vile klorini. Dutu hii ni kioksidishaji madhubuti na humenyuka kwa ukali sana iwapo na maunzi yanayoweza kuwaka na yanayonakisi. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na misombo mingi, kusababisha athari ya moto na mlipuko. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya vumbi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Hutengana chini ya kiwango myeyuko ifikapo 230°C Uzito wiani (maji = 1): >1 Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 25 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa maji.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Pia shauriana na ICSC0126 Klorirni.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||