1,2-DICHLOROETHYLENE ICSC: 0436
Mei 2003

1,2-Dichloroethene
Acetylene dichloride
symmetrical Dichloroethylene
CAS # 540-59-0 C2H2Cl2 / ClCH=CHCl
RTECS # KV9360000 Masi ya molekuli: 96.95
UN # 1150
EC # 602-026-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, mnyunyizio wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kusinzia. Udhaifu. Kupoteza fahamu. Kutapika.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga mkavu au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Ainisho ya EU
Alama: F, Xn
R: 11-20-52/53
S: (2-)-7-16-29-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30GF1-I+II
Msimbo wa NFPA: H 2; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kilichofungwa vizuri. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,2-DICHLOROETHYLENE ICSC: 0436
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapoathiriwa na hewa, mwanga na unyevu huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka pamoja na shaba au mchanganyiko wa shaba na madini mengine, na besi kuunda sumu ya kloroasetilini ambayo huwaka yenyewe inapokutana na hewa. Hushambulia plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 200 ppm kama TWA; (ACGIH 2003).
MAK: 200 ppm, 800 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Mchanganyiko unaoweza kudhuru yaweza kutokea kama dutu hii inavukiza kwa hewa yenye joto ya 20°C kufikiwa kwa haraka na hata kama inanyunyizwa au inatawashika huwa kwa haraka zaidi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kwa mfiduo wa viwango vya juu kusababisha kupungua kwa fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 55°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.28
Umumunyifu katika maji: mbaya
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.34
Kiwango cha kumweka: 2°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 460°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 9.7-12.8
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii ina isoma mbili, cis na trans. Viwango viwili vya kiwango kwa mfuatano vinahusu isoma za cis na trans: isoma ya cis (CAS 156-59-2), isoma ya trans (CAS 156-60-5); kiwango mchemko 60.3, kiwango myeyuko -81.5°C (cis), -49.4°C (trans); kiwango cha kumweka c.c. 6°C (cis), 2-4°C (trans); uzitowiani wa mvuke (hewa = 1) 1.28 (cis), 1.26 (trans); kanieneo mvuke 24.0 kPa (cis), 35.3 kPa (trans) at 20°C; uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.6 (cis), 1.8 (trans); oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.86 (cis), 2.09 (trans). Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005