CYCLOHEXANONE ICSC: 0425
Aprili 2004

Ketohexamethylene
Pimelic ketone
Cyclohexyl ketone
CAS # 108-94-1 C6H10O
RTECS # GW1050000 Masi ya molekuli: 98.14
UN # 1915
EC # 606-010-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu linalokinza alkoholi, dioksidi kaboni, poda.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 44°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 44°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kusinzia.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni. Vazi linalokinga kemikali.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 10-20
S: (2-)-25
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1915.
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CYCLOHEXANONE ICSC: 0425
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, kama vile asidi nitriki, kusababisha athari ya moto na mlipuko.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 20 ppm kama TWA; 50 ppm kama STEL; (ngozi); A3; (ACGIH 2004).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; (DFG 2004).
EU OEL: 10 ppm kama TWA; 20 ppm kama STEL; (ngozi); (EU 2000).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Mfiduo juu ya OEL husababisha kupungua fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 156°C
Kiwango myeyuko: -32.1°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.95
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 8.7
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 500
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.4
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 44°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 420°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.1 (ifikapo 100°C) -9.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.81
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005