| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
|
|
Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Kisichoingiza hewa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 21-25-36/38-43 S: (1/2-)-3-22-36/37-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-III Msimbo wa NFPA : H 4; F 1; R 3; |
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE ISO IMARA, ISO RANGI, HUNYONYA MAJI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kwenye joto zaidi ya 122°C. Dutu hii hutengana inapopata joto zaidi ya 49°C, inapogusana na asidi, besi na unyevu huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni na sianidi. Humenyuka pamoja na asidi, vioksidishaji vikali, kinakisishaji kikali na maji kusababisha athari ya mlipuko na yenye sumu. Hushambulia metali nyingi. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 mg/m³ kama TWA (ACGIH 2004). MAK: 1 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); kuhisisha ngozi (Sh); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri ini. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko ifikapo 0.067kPa: 83°C Kiwango myeyuko: 45-46°C Uzito wiani (maji = 1): 1.3 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 15°C: 77.5 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.45 |
Kiwango cha kumweka: 141 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
pH ifaayo kwa kuhifadhi mimumunyo ni karibu 4; mimumunyo inaweza kuhifadhiwa katika glasi ili mradi imeimarishwa na asidi fosforiki, asetiki, salfuriki au boriki. Viwango wa mchemko vinginevyo: 140°C ifikapo 2.5 kPa. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Sianamidi hutumika pia kumaanisha sianamidi kalsiamu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||