| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mwendo wa kuyumbayumba. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Degedege. Kupoteza fahamu. Tazama Vidokezo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
|
| Macho |
(Tazama Ngozi).
|
Miwanivuli ya usalama, kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F+, Xn R: 12-40-48/20 S: (2-)-9-16-33 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1063 au 20G2F Msimbo wa NFPA : H 2; F 4; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU, ISO RANGI HATARI KWA MWILI: Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile kloridi hidrojeni na fosjini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na poda za alumini na zinki, trikloridi alumini na ethilini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia metali nyingi endapo kuna unyevu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 50 ppm kama TWA, 100 ppm kama STEL; (ngozi); A4; (ACGIH 2004). MAK: 50 ppm, 100 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia kwenye ngozi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Kioevu hiki huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo huweza kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kuleta uharibifu wa ini, mfumo wa moyo na mishipa, na mafigo. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, kusababisha matokeo yanayopima vya tabia. Majaribio kwa wanyama yanaonyesha kuwa dutu hii huenda ikasababisha athari za sumu kwa uzazi wa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -24.2°C Kiwango myeyuko: -97.6°C Uzito wiani (maji = 1): 0.92 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.5 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 21°C: 506 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.8 |
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo Jotoridi la kujiwasha: 632°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 8.1-17.4 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.91 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kufuatia kuleshwa, mgonjwa lazima achunguzwe vizuri kwa masaa 48. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||