SULFUR MUSTARD ICSC: 0418
Aprili 2005

HD
Mustard gas
Bis(2-chloroethyl)sulfide
1,1'-Thiobis(2-chloroethane)
CAS # 505-60-2 C4H8Cl2S
RTECS # WQ0900000 Masi ya molekuli: 159.1
UN # 2810
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka katika hali mahususi.
Usiwashe moto.
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi. Mchomo. Kuumwa koo. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Huduma ya kusaidia kupumua ya mdomo kwa mdomo hairuhusiwi. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko nzito ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Vaa glavu za kinga unapotoa huduma ya kwanza. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Kutoa machozi. Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu wa kudumu.
Miwanivuli ya usalama, na kingao cha uso, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. Mchomo. Mshtuko au kuzimia. (Tazama Kuvuta pumzi).
Nawa mikono kabla ya kula. Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Usimtapishe. Usitoe msaada wa kupumua kwa kupuliza mdomo kwa mdomo. Tumia oksijeni inayotolewa na wataalamu. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-I
Msimbo wa NFPA: H 4; F 1; R 1; 0
Kinachotenganishwa na maji, vyakula na malisho. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu. Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SULFUR MUSTARD ICSC: 0418
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO KAMA MAFUTA AU FUWELE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yenye sumu. Humenyuka pamoja na maji. Hushambulia metali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
MAK: H Aina ya sarakani: 1; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Husababisha malengelenge. Inayotoza machozi. Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi yenye dutu hii kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu. Dutu hii huweza kuathiri macho kusababisha kuharibika kwa utendaji. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 216°C
Kiwango myeyuko: 13.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.27
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.0068 ni dhaifu
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 9.33
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.5
Kiwango cha kumweka: 105°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.37-2.41
DATA YA MAZINGIRA
Kuendelea kwa kemikali hii kunaweza kuwa katika udongo na theluji.
VIDOKEZO
Usichukue nguo za kazi nyumbani. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Yperite, Lost ni jina la kawaida.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005