| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
|
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge. INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
|
Glavu za kuhami baridi. Mavazi ya kinga.
|
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
|
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. Ondoa gesi kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linaloruhusu gesi linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Ainisho ya EU Alama: T, N R: 10-23-34-50 S: (1/2-)-9-16-26-36/37/39-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3 Jasara tanzu za UN: 8 | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20S1005 au 20G2TC Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 0; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji, asidi, halojeni. Baridi. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI, YENYE HARUFU KALI. HATARI KWA MWILI: Gesi ni nyepesi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa zebaki, fedha na oksidi dhahabu. Dutu hii ni besi kali humenyuka vikali ikiwa na asidi na husababisha ulikaji. Humenyuka vikali ikiwa na vioksidishaji vikali na halojeni. Hushambulia shaba, alumini, zinki na aloi zake. Humumunyika majini na kutoa joto. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 25 ppm kama TWA; 35 ppm kama STEL; (ACGIH 2004). MAK: 20 ppm, 14 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi wa viwango vya juu kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: -33°C Kiwango myeyuko: -78°C Uzito wiani (maji = 1): 0.7 ifikapot -33°C Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 54 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 26°C: 1013 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 0.59 |
Jotoridi la kujiwasha: 651°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 15-28 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||