| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: usitumie maji, vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Mchomo. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Msokoto wa tumbo. Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Kutapika.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Usimpe chochote cha kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vikavu. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: III | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
|
Kinachotenganishwa na asidi kali, vikaboni, maji, vyakula na malisho. Kavu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE RISHAI, NYEUPE HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo huu katika maji ni besi kali ya kati. Humenyuka pamoja na maji kutoa joto la kutosha kuwasha vitu viwakavyo. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na asidi, halojeni, metali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 mg/m³ kama TWA (ACGIH 2004). MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo) (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu kwa chembe za vumbi. Dutu hii husababisha vidonda na utoboaji wa septamu ya pua. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 2850°C Kiwango myeyuko: 2570°C Uzito wiani (maji = 1): 3.3-3.4 Umumunyifu katika maji: mmenyuko |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. Mabonge ya oksidi kalsiamu yanayotokana na utendaji wa unyevuunyevu na protini kwenye macho ni vigumu kuyatoa kwa mnyunyizo wa maji. Ni lazima daktari ayatoe mwenyewe. KAMWE usimiminie maji dutu hii; wakati wa kumumunyisha au kuzimua, daima itie polepole kwenye maji.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||