CALCIUM CARBIDE ICSC: 0406
Oktoba 1995

Calcium acetylide
Acetylenogen
CAS # 75-20-7 CaC2
RTECS # EV9400000 Masi ya molekuli: 64.1
UN # 1402
EC # 006-004-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki lakini hutengeneza gesi inayoungua ikigusana na maji au hewa nyevunyevu. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usigusishe na maji.
Poda maalum, mchanga mkavu, USITUMIE kitenzi kingine.
MLIPUKO Hatari ya moto na mlipuko ianpogusana na maji.
Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa n.k. kwa kunyunyizia maji BILA (vilivyomo) kugusa maji.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kupumua kwa shida. Mshtuko au kuzimia. (Tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari. Tazama Vidokezo.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Zoa dutu iliyomwagika katika vyombo vikavu. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usitumie maji.
Kisichoingiza hewa.
Ainisho ya EU
Alama: F
R: 15
S: (2-)-8-43
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 4.3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 43GW2-1
Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 2; W
Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana (tazama Hatari za Kikemikali). Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CALCIUM CARBIDE ICSC: 0406
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE KIJIVU AU MABONGE MYEUPE, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Misombo isiyohimili mshtuko hutengenezwa kwa nitrati silva na chumvi za shaba. Dutu hii hutengana kwa ukali sana inapogusana na unyevuunyevu na maji huzalisha gesi ziwakazo asetilini (ICSC 0089), kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na klorini, bromini, iodini, kloridi hidrojeni, risasi, floridi, magnesiamu, peroksidi sodiamu na sulfuri kusababisha athari ya moto na mlipuko. Michanganyiko ya feri(III) kloridi, feri(III) oksidi na bati(II) kloridi italipuka na huungua kwa nguvu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Hubabua. Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo).

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: takribani 2300°C
Uzito wiani (maji = 1): 2.22
Umumunyifu katika maji: mmenyuko
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Humenyuka kwa nguvu na vitenzi vya kuzimia moto kama vile maji. The substance may contain contaminant resulting in the release of the toxic gas phosphine on contact with water. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pia shauriana na ICSC #0089 (asetilini).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005