CADMIUM SULFIDE ICSC: 0404
Aprili 1997

Cadmium monosulfide
CAS # 1306-23-6 CdS
RTECS # EV3150000 Masi ya molekuli: 144.5
UN #
EC # 048-010-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kikohozi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kuhara. Kichefuchefu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 45-22-48/23/25-62-63-68
S: 53-45-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
CADMIUM SULFIDE ICSC: 0404
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO ISIYOKOZA AU RANGI YA MACHUNGWA AU PODA MANJANO HADI KAHAWIA

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za sulfuri. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka pamoja na asidi na kutoa gesi yenye sumu (sulfidi hidrojeni).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: (vumbi) 0.01 mg/m³; (sehemu pumuzi) 0.002 mg/m³ as TWA; A2; BEI imetolewa; (ACGIH 2005).
MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mapafu huathirika na mfiduo unaorudiwa au wa muda mrefu. Dutu hii huweza kuathiri mafigo na mifupa, kusababisha kuharibika kwa figo na udhaidu wa mifupa. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango usablimishaji: 980°C
Uzito wiani (maji = 1): 4.8
Umumunyifu katika maji: hakuna
DATA YA MAZINGIRA
Katika mfuatano wa ulishano ambao ni muhimu kwa binadamu, mlimbikizo wa kibiliolojia hutokea, hasa kwenye wanyama na wadudu wenye magamba, mimea. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Maelezo ni machache kuhusu matokeo ya dutu hii. Matokeo ya afya baada ya uchunguzi wa misombo ya kadimiamu. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Kuchomea au kulehemu nyuso zenye salfidi kadimiamu hutoa oksidi kadimiamu yenye sumu kali inayoweza kudhuru mapafu (tazama ICSC 0117 Monoksidi kadimiamu). Usichukue nguo za kazi nyumbani. Cadmium golden 366, Cadmium lemon yellow, Cadmium orange, Cadmium primrose 819, Cadmium yellow 10G conc, Cadmium yellow conc. primrose, Cadmopur golden yellow N, Cadmopur yellow, Capsebon, Ferro lemon yellow ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005