BUTYRALDEHYDE ICSC: 0403
Machi 1996

Butanal
Butyl aldehyde
CAS # 123-72-8 C4H8O / CH3-CH2-CH2-CHO
RTECS # ES2275000 Masi ya molekuli: 72.1
UN # 1129
EC # 605-006-00-2
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Povu, povu linalokinza alkoholi, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka. Ukanzaji unaweza kusababisha ongezeko la kanieneo na kuleta athari ya kupasuka na kulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mchomo.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Alama: F
R: 11
S: (2-)-9-29-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1129 au 30GF1-I+II
Msimbo wa NFPA: H 3; F 3; R 2;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na maunzi yasiokubaliana: tazama Hatari za Kikemikali. Baridi. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
BUTYRALDEHYDE ICSC: 0403
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU KALI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Dutu hii huweza kupolimisha kutokana na kukanza kwa kuathiriwa na asidi au alkali. Humenyuka pamoja na amini, vioksidishaji, besi na asidi kali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 75°C
Kiwango myeyuko: -99°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.8
Umumunyifu katika maji, g/100 ml: 7
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 12.2
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5
Kiwango cha kumweka: -7°C
Jotoridi la kujiwasha: 230°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.5-12.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.18
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005