trans-2-BUTENE ICSC: 0398
Machi 1996

2-Butene, (E)-
trans-Dimethylethylene
beta-trans-Butylene
(silinda)
CAS # 624-64-6 C4H8 / CH3-HC=CH-H3
RTECS # Masi ya molekuli: 56.1
UN # 1012
EC # 601-012-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia mnyunyizo wa maji.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza) ikiwa ni kioevu. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche. Kwa kuzuia moto kuingia kwenye silinda tumia vizimio vya miali ya moto.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Tazama Ngozi.
Kingao cha uso.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. KAMWE usielekeze nyiri ya maji juu ya kioevu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Ainisho ya EU
Alama: F+
R: 12
S: (2-)-9-16-33
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-20S1012 au 20G2F
Msimbo wa NFPA : H 1; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Hifadhi nje au mahali pa peke yake, yengo lenye hewa ya kutosha. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
trans-2-BUTENE ICSC: 0398
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI OEVU ILIYOBANWA, ISO RANGI

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana, na huweza kujilimbikiza katika eneo ambalo dari liko chinichini na kusababisha upungufu wa oksijeni. Kutokana na mtiririko, mchukucho n.k., chaji za kiumemetuamo huweza kutokea.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kisipodhibitiwa kioevu hiki huvukiza haraka sana na kusababisha ukifishwaji mno wa hewa na kuleta hatari kubwa ya kukosekana hewa katika maeneo funge.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Uvukizaji wa haraka wa kioevu huweza kusababisha jamidi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo huweza kusababisha kupoteza fahamu.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 1°C
Kiwango myeyuko: -105°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.6
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 212
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.9
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Jotoridi la kujiwasha: 324°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.8-9.7
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.31
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Ukolezi mkubwa katika hewa husababisha unakisi wa oksijeni pamoja na hatari ya kupoteza fahamu au kufa. Pima kiasi cha oksijeni kabla ya kuingia katika eneo. Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu cis-2-butene (ICSC # 0397). .
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005