1,2-BUTANEDIOL ICSC: 0395
Machi 1996

1,2-Butylene glycol
1,2-Dihydroxybutane
CAS # 584-03-2 C4H10O2 / CH3CH2CH(OH)CH2OH
RTECS # EK0380000 Masi ya molekuli: 90.1
UN #
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 90°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 90°C, uingizaji hewa.

MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko.
Ngozi
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA : H 1; F 2; R 0;
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
1,2-BUTANEDIOL ICSC: 0395
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI KINATACHO

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho. Mfiduo wa viwango vya juu husababisha kupungua fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri mafigo (kwa kumeza), kusababisha vidonda vya tishu na kuharibika kwa figo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 194°C
Kiwango myeyuko: -114°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.01
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 10
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00
Kiwango cha kumweka: 90°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005