| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE! EPUKA MFIDUO KWA WANAWAKE (WAJAWAZITO)!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua. Kuumwa kichwa. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Udhaifu. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo). (Tazama Kumeza).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Ngozi kavu. Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Madhara kwa kiwambo ute cha jicho.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Mchomo. Kutapika. Kichefuchefu. Maumivu ya tumbo. Msokoto wa tumbo. Kuhara. Mipasuko ya misuli. Mshtuko. Kifo.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T+, N R: 45-28-34-50/53 S: 53-45-60-61 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-II Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 2; |
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho, vinakisishaji vikali.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MABONGE MYEUPE AU ANGAVU, AU PODA FUWELE HATARI ZA KIKEMIKALI: Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu ambayo yaweza kutendana na dutu kinakisishaji kufanyiza gesi yenye sumu kali (arsini - ICSC # 0222). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.01 mg/m³ kama TWA; A1); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva na ini. Mfiduo huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo). Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya upumuaji, ngozi (hyperkeratosis), uboho (mabadiliko katika damu), mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva na ini, kusababisha anemia na kuharibika kwa utendaji. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 457-465°C Kiwango usablimishaji: 193°C Kiwango myeyuko: 275-313°C Uzito wiani (maji = 1): 3.7-4.2 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 1.2-3.7 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa ndege, samaki na mamalia.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Tabia za kimaumbile zinategemea hali ya fuwele ya dutu hii. Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Dalili za papo hapo za sumu hutokea kati ya saa ½ na saa 1 baada ya mfiduo lakini dalili zaweza kuchelewa kwa masaa kadhaa. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu misombo ya trivalenti arseniki iso-kikaboni (arsenites).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||