| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Udhaifu. Maumivu kifuani. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Mchomo. Maumivu.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kutapika. Kiu kali. Mipasuko misuli. Mshtuko. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Ondoa chembe zinazosafirishwa kwa hewa kwa mnyunyuzio mwembamba wa maji. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 45-23/25-50/53 S: 53-45-60-61 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT5-II Msimbo wa NFPA : H 2; F 0; R 0; |
Kinachotenganishwa na besi kali, vinakisishaji, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA NYEUPE, RISHAI HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa zaidi ya 300°C huzalisha mafusho yenye sumu (trioksidi arseniki - ICSC 0378) na oksijeni. Mmumunyo huu katika maji ni asidi dhaifu. Humenyuka vikali ikiwa na pentafloridi bromini kusababisha athari ya moto na mlipuko. Humenyuka pamoja na kinakisishaji, kufanyiza gesi yenye sumu kali (arsini - ICSC 0222). Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji au unyevuunyevu. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 0.01 mg/m³ kama TWA; A1); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 1; Aina inayoleta mabadiliko kwa seli za uzazi: 3A; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri damu, mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva wa pembeni na ini. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo). Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri ngozi (hyperkeratosis), mfumo wa moyo na mishipa, mfumo wa neva wa pembeni, uboho (mabadiliko katika damu), ini na mapafu. Dutu hii husababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango myeyuko (hutengana): 315°C Uzito wiani: 4.3 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 65.8 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe na viumbe hai vya majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Dalili za papo hapo za sumu hazijitokezi mpaka saa kadhaa baadaye. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Hakuna onyo la harufu iwapo kuna vikolezi vya kitoksini. Usichukue nguo za kazi nyumbani. Mapendekezo kwenye kadi hii pia yanahusu misombo ya pentavalenti arseniki iso-kikaboni (arsenates).
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||