n-BUTYLAMINE ICSC: 0374
Oktoba 1997

1-Aminobutane
1-Butanamine
Monobutylamine
CAS # 109-73-9 C4H11N / CH3(CH2)3NH2
RTECS # EO2975000 Masi ya molekuli: 73.1
UN # 1125
EC # 612-005-00-0
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, maji mengi, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Kikohozi. Mchomo. Kuumwa kichwa. Kujisikia joto na kujaa usoni. Kutapika. Kizunguzungu. Kukosa pumzi. Kupumua kwa shida. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Maumivu. Wekundu. Malengelenge. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana. Upofu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Maumivu ya tumbo. Kuhara. Kichefuchefu. Kutapika. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: F, C
R: 11-20/21/22-35
S: (1/2-)-3-16-26-29-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Jasara tanzu za UN: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1125 au 30GFC-II
Msimbo wa NFPA : H 3; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
n-BUTYLAMINE ICSC: 0374
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HUGEUKA NJANO IKIKAA KWA MUDA.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Dutu ni besi dhaifu. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali na asidi kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia baadhi ya metali iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm (kiwango cha juu); (ngozi); (ACGIH 2004).
MAK: 5 ppm, 15 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 78°C
Kiwango myeyuko: -50°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.74
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 10.9
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.5
Kiwango cha kumweka: -12°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 312°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.7-9.8
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.86
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005