ALACHLOR ICSC: 0371
Oktoba 1999

2-Chloro-2',6'-diethyl-N-(methoxymethyl)acetanilide
CAS # 15972-60-8 C14H20ClNO2
RTECS # AE1225000 Masi ya molekuli: 269.8
UN #
EC # 616-015-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Michanganyiko ya vioevu vyenye vimumunyisho vya kaboni huweza kuwaka (moto).
Usiwashe moto.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi
Uingizaji hewa (hapana kama ni poda), mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
Macho
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. Vuta kiombwe maunzi yaliyomwagika. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn, N
R: 22-40-43-50/53
S: (2-)-36/37-46-60-61
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hatari ya kuzuia mmiminiko kutoka kwenye kizimamoto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Usihifadhi karibu na joto au mwalimoto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ALACHLOR ICSC: 0371
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO FUWELE, ISO HARUFU, ISO RANGI HADI RANGI KAMA MAZIWA.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza gesi zenye sumu: monoksidi kaboni (ICSC0023), oksidi za nitrojeni, kloridi hidrojeni (ICSC0163).

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki MAK haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza au inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri ini. Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 40°C
Uzito wiani: 1.1g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: hakuna
Kiwango cha kumweka: 137°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.5
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini. Epusha kuingia katika mazingira tofauti na matumizi ya kawaida.
VIDOKEZO
Vimumunyishaji chukuzi vitumikavyo katika misombo ya kibiashara vyaweza kubadilisha tabia za kimaumbile na za kitoksini.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005