| |||||||||||||
| |||||||||||||
|
|||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka.
|
Usiwashe moto.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi. Zuia mlimbiko wa chaji za umemetuamo (k.m. kwa kutuliza).
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kuumwa koo.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo plastiki; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi.
|
Ainisho ya EU Alama: Xi R: 36 S: (2-) Ainisho ya UN | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Msimbo wa NFPA : H ; F 1; R 0;
|
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: PODA FUWELE ISO RANGI, ISO HARUFU HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. Iwapo kavu, huweza kuchajiwa kiumemetuamo kwa kuzinga, upitishaji nyumatiki, umiminaji, nk. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi kama vile asidi ya valeri na dutu nyinginezo. Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka pamoja na viosidishaji. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 5 mg/m³ kama TWA; (ACGIH 1997). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi ya erosoli yake kunaweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo). ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 338°C Kiwango myeyuko: 152°C Uzito wiani: 1.36 g/ml Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 15°C: 1.4 (wastani) Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 18.5°C: 10 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.04 |
Kiwango cha kumweka: 196°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 422°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.08 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||