ETHYL ACETATE ICSC: 0367
Oktoba 1997

Acetic acid, ethyl ester
Acetic ether
CAS # 141-78-6 C4H8O2 / CH3COOC2H5
RTECS # AH5425000 Masi ya molekuli: 88.1
UN # 1173
EC # 607-022-00-5
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua sana.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. Tumia vifaa vya mkono visivyotoa cheche.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kuumwa koo. Kupoteza fahamu. Udhaifu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
Ainisho ya EU
Alama: F, Xi
R: 11-36-66-67
S: (2-)-16-26-33
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1173
Msimbo wa NFPA : H 1; F 3; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ETHYL ACETATE ICSC: 0367
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Kukanza kunaweza kusababisha mwako au mlipuko mkali. Dutu hii hutengana inapoathiriwa na mwanga wa urujuani iliyokoza (UV), besi, asidi. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, besi au asidi. Hushambulia alumini na plastiki.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 400 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: 400 ppm, 1500 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 77°C
Kiwango myeyuko: -84°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji: vizuri sana
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 10
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0
Kiwango cha kumweka: -4°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 427°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.2-11.5
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.73
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Acetidin, Vinegar naphtha ni majina ya kibiashara.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005