2-ETHOXYETHYL ACETATE ICSC: 0364
Novemba 2003

Ethylene glycol monoethyl ether acetate
2-Ethoxyethanol acetate
Acetic acid, 2-ethoxyethyl ester
Cellosolve acetate
Ethyl glycol acetate
CAS # 111-15-9 C6H12O3 / CH3COOCH2CH2OCH2CH3
RTECS # KK8225000 Masi ya molekuli: 132.2
UN # 1172
EC # 607-037-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizio wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 51.1°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 51.1°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kizunguzungu. Kusinzia. Kuumwa kichwa. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! Ngozi kavu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Uingizaji hewa. Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 60-61-20/21/22
S: 53-45
Angalia: [E]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1172
Msimbo wa NFPA: H 1; F 2; R ;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, besi kali, asidi kali. Weka gizani.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-ETHOXYETHYL ACETATE ICSC: 0364
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii huenda ikatengeneza peroksidi lipukaji. Humenyuka pamoja na asidi kali, besi kali, vioksidishaji vikali.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 5 ppm, 27 mg/m³, kama TWA; (ngozi); (ACGIH 2003).
MAK: 5 ppm, 27 mg/m³; kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya kiwango cha juu: II(8); Kundi la waja wazito lililo hatarini: B; (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Mvuke huu inakera kwa upole macho. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha vidonda vya seli za damu na kuharibika kwa figo (mfiduo wa viwango vya juu). Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kupoteza fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha vidonda vya seli za damu, anemia na kuharibika kwa figo. Inaweza kusababisha kusumisha kwa uzazi na kukua kwa binadamu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 156°C
Kiwango myeyuko: -62°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.97 (ifikapo 20°C)
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 23
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.27
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.7
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01)
Kiwango cha kumweka: 51.1°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 379°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.3-14
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.24
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kagua kama kuna peroksidi kabla ya kunereka; iwapo chanya fanya iwe salama.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005