ACETIC ACID ICSC: 0363
Oktoba 1997

Glacial acetic acid
Ethanoic acid
Ethylic acid
Methanecarboxylic acid
CAS # 64-19-7 C2H4O2 / CH3COOH
RTECS # AF1225000 Masi ya molekuli: 60.1
UN # 2789 (>80%)
EC # 607-002-00-6
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, povu linalokinza alkoholi, mnyunyizo wa maji, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 39°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 39°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Mchomo. Kikohozi. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Kuumwa koo. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Mibabuko ya ngozi. Maumivu. Malengelenge.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Upofu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Mchomo. Kuhara. Mshtuko au kuzimia. Kuumwa koo. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Katisha kioevu kilichomwagika kwa uangalifu chini ya uangaliziwa mtaalam kutumia kabonati sodiamu, chini ya mamlaka mjuzi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia).
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 10-35
S: (1/2-)-23-26-45
Angalia: [B]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Jasara tanzu za UN: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S2789 au 80GCF1-II
Msimbo wa NFPA : H 2; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ACETIC ACID ICSC: 0363
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii ni asidi dhaifu. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji na besi. Hushambulia metali nyingi na kutoa gesi inayoweza kuwaka/lipukaji (Hidrojeni - tazama ICSC 0001). Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 10 ppm kama TWA, 15 ppm kama STEL; (ACGIH 2004).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo) (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii na mvuke huu husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya mvuke wake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Dutu hii huweza kuathiri njia ya utumbo, kusababisha msago wa chakula pamoja na yabisi na kufunga tumbo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 118°C
Kiwango myeyuko: 16.7°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.05
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 1.5
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 2.1
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.02
Kiwango cha kumweka: 39°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 427°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 5.4-16
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: -0.31
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya mnyunyuzio mwafaka unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Nambari nyingine za UN: UN 2790 mmumunyo wa asidi asetiki (10-80% asidi asetiki); ainisho ya UN ya hatari 8.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005