STODDARD SOLVENT ICSC: 0361
Aprili 2004

White spirit
CAS # 8052-41-3
RTECS # WJ8925000
UN # 1268
EC # 649-345-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 21°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 21°C, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Uchovu. Kizunguzungu. Kuchanganyikiwa. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Ngozi kavu. Wekundu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Kichefuchefu. Kutapika. Maumivu ya tumbo. Kuhara. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Usimtapishe. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 45-65
S: 53-45
Angalia: [H na P]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1268
Msimbo wa NFPA: H 1; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
STODDARD SOLVENT ICSC: 0361
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali kusababisha athari ya moto na mlipuko. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira, na mipako.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 100 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na ngozi. Kuvuta pumzi yenye mvuke wake kunaweza kusababisha mkereketo wa macho na sehemu ya njia ya kuingizia hewa. Kumeza kioevu hiki kunaweza kusababisha madhara kwenye mapafu kukifyonza na kunaweza kuleta kichomi kinachotokana na kemikali. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva. Mfiduo wa mvuke wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 130-230°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.765-0.795
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.1-1.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 4.5-5
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.01
Kiwango cha kumweka: 21°C (tazama Vidokezo)
Jotoridi la kujiwasha: 230-240°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 0.6-8.0
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 3.16-7.06
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Huu ni mchanganyiko wa hidrokaboni alifatiki na alisikliki (C7-C12), na hidrokaboni aromatiki (C7-C12). Inaweza kuwa na benzini (tazama ICSC0015) lakini vimumunyishaji vya kisasa vya Stoddard kwa kawaida huwa na benzini kidogo au havina kabisa. Dalili za ugonjwa wa mapafu na kemikali kwa kawaida hazijitokezi mpaka mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Jotoridi la kujiwasha laweza kushushwa hadi kukaribia 180°C kukiwepo na maunzi yenye eneo kubwa la uso. Kiwango cha kumweka hutofautiana 21 hadi 60 °C kulingana na vichanganyio.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005