| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Mgusano na unyevu au maji unaweza kutoa joto la kutosha kuwasha dutu za kuwasha.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Inabaua. Mchomo. Kuumwa koo. Kikohozi. Kupumua kwa shida. Kukosa pumzi. Dalili zinaweza kuchelewa (tazama Vidokezo).
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Inabaua. Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi nzito. Malengelenge.
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Inabaua. Wekundu. Maumivu. Kiwaa. Kuungua kunakopenya sana.
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Inabaua. Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombosuitable; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Osha salio kwa maji mengi. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: C R: 35 S: (1/2-)-26-37/39-45 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 8 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80S1823 au 80GC6-II+III Msimbo wa NFPA : H 3; F 0; R 1; |
Kinachotenganishwa na asidi kali, metali, vyakula na malisho. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi kwenye eneo lenye sakafu isiyolika.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: MANGO NYEUPE, OEVU KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, ISO HARUFU. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii ni besi kali humenyuka vikali ikiwa na asidi na husababisha ulikajihadi metali hasa kwenye unyevuunyevu kama vile zinki, alumini, bati na risasi, kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni ICSC0001). Humenyuka pamoja na chumvi za amonia kufanyiza amonia, kusababisha athari ya moto. Hushambulia aina fulani za plastiki, mpira au mipako. Hufyonza haraka dioksidi kaboni na maji toka hewani. Mgusano na unyevu au maji unaweza kutoa joto (tazama Vidokezo). VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 mg/m³ (kiwango cha juu) (ACGIH 2000). MAK haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Hubabua. Dutu hii husababisha ulikaji vibaya kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa. Kuvuta pumzi ya erosoli yake kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 1390°C Kiwango myeyuko: 318°C Uzito wiani: 2.1 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 109 |
|||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inaweza kuwa na madhara kwa mazingira; tahadhari maalumu itolewe kwa viumbe hai vya majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. KAMWE usimiminie maji dutu hii; wakati wa kumumunyisha au kuzimua, daima itie polepole kwenye maji. Nambari nyingine za UN: UN1824 Sodium hydroxide solution, ainisho ya hatari 8.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||