SODIUM METASILICATE (ANHYDROUS) ICSC: 0359
Aprili 2004

Silicic acid, sodium salt
Disodium metasilicate
Disodium trioxosilicate
CAS # 6834-92-0 Na2SiO3
RTECS # VV9275000 Masi ya molekuli: 122.1
UN # 3253
EC # 014-010-00-8
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
Kuvuta pumzi Kuumwa koo. Mchomo. Kikohozi. Kukosa pumzi.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu. Mibabuko ya ngozi.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia iwapo poda.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Mchomo. Maumivu ya tumbo. Mshtuko au kuzimia.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vya plastiki; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Katisha salio kwa uangalifu na asidi iliyozimuliwa (pendelea asidi asetiki). Kisha osha kwa maji mengi. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: C
R: 34-37
S: (1/2-)-13-24/25-36/37/39-45
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 8
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 80GC6-II+III
Kinachotenganishwa na asidi kali, vyakula na malisho, metali, halojeni. Hifadhi mahali penye sakafu isiyoshika kutu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
SODIUM METASILICATE (ANHYDROUS) ICSC: 0359
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
MANGO KATIKA MAUMBO MBALIMBALI, ISIYO NA RANGI HADI NYEUPE, YA RISHAI

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Mmumunyo huu katika maji ni besi kali, humenyuka vikali ikiwa na asidi na husabisha ulikaji hadi alumini, zinki, na kutoa gesi inayoweza kuwaka/kulipuka (hidrojeni - tazama ICSC 0001). Humenyuka pamoja na halojeni kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki. MAK haijathibitishwa.
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka inapotawanywa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii husababisha ulikaji kwa macho, ngozi na njia ya upumuaji. Husababisha ubabuzi inapomezwa.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 1089°C
Uzito wiani: 2.6 g/cm³
Umumunyifu katika maji: vizuri
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO

MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005