ROSIN ICSC: 0358
Aprili 2004

Colophony
Gum rosin
CAS # 8050-09-7
RTECS # VL0480000
UN #
EC # 650-015-00-7
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizo wa maji, poda.
MLIPUKO


MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho
Miwanivuli ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.

KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P2 cha chembe zinazodhuru.
Ainisho ya EU
Alama: Xi
R: 43
S: (2-)-24-37
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI

Hifadhi katika viwekeo vilivyofunikwa. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
ROSIN ICSC: 0358
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
PODA AU VIPANDE MANJANO ISIYOKOZA HADI ILIYOIVA, YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa kuzalisha mafusho yakerayo.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: Kama matokeo ya rosini zilizoyeyushwa kwa joto (asidi ya resini). Kuwepo kwake kwa njia zote udhibitiwe hadi kufikia kiwango cha chini iwezekanavyo. SEN; (ACGIH 2004).
MAK: kuhisisha ngozi (Sh); (DFG 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi yenye mafusho.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe ya dhuru yaweza kufikiwa haraka inapotawanywa hasa iwapo katika hali ya poda au mafusho.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango myeyuko: 100-150°C
Uzito wiani: 1.07 g/cm³
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kiwango cha kumweka: 187°C
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Rosini hutokana na mti wa mpaini. Rosini inapatikana kama rosini ya mbao, gundi au mafuta. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005