GLUTARALDEHYDE (50% SOLUTION) ICSC: 0352
Aprili 2000

1,5-Pentanedial (50% solution)
CAS # 111-30-8 C5H8O2 / HCO(CH2)3CHO
RTECS # MA2450000 Masi ya molekuli: 100.1
UN # 2810
EC # 605-022-00-X
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua. Kuumwa koo.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Ukwaru. Mibabuko ya ngozi. Malengelenge. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu. Maumivu. Kuungua kunakopenya sana.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Osha salio kwa maji mengi. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T, N
R: 23/25-34-42/43-50
S: (1/2-)-26-36/37/39-45-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-II
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
GLUTARALDEHYDE (50% SOLUTION) ICSC: 0352
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, ANGAVU, CHENYE HARUFU KALI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.05 ppm (kiwango cha juu); A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); SEN (ACGIH 2004).
MAK: 0.05 ppm, 0.21 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: I(2); uhisishaji wa koromeo la hewa na ngozi (Sah); Aina ya sarakani: 4; Kundi la waja wazito lililo hatarini: C; (DFG 2005).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru waweza kufikiwa polepole kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera sananjia ya upumuaji na husababisha ulikaji kwa macho na ngozi.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi. Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu (tazama Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 101°C
Kiwango myeyuko: -6°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.1
Umumunyifu katika maji: kuchanganyika
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 2.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.05
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini.
VIDOKEZO
Kikomo thamani cha mfiduo matumizi ya kazi kisivukwe wakati wowote wa mfiduo amilifu. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Pia shauriana na ICSC #0158 Glutaraldehyde.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005