| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huungua sana.
|
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
|
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Michanganyiko ya mvuke/hewa hulipuka.
|
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka. USITUMIE hewa iliyoshindiliwa kujaza, kutoa au kuchukua.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA UTOKAJI WA UKUNGU!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Kikohozi. Kukosa pumzi. Kuumwa koo.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
Wekundu. Malengelenge.
|
Glavu za kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu. Miunguzo midogo.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Kusinzia. Kuumwa kichwa.
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja katika vyombo vinavyozibika. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Usielekeze kwenye mfereji wa maji machafu. (Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Ainisho ya EU Alama: F R: 11 S: (2-)-16-23-29-33 Angalia: [D] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 3 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 30S1301 Msimbo wa NFPA : H 2; F 3; R 2; |
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali. Baridi. Kavu. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Hifadhi iwapo tu imetulia.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI, KIMIMINIKA, CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii huweza kupolimisha kirahisikutokana na kupata joto au kwa kuathiriwa na mwanga au peroksidi kwa athari ya moto au mlipuko. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na vioksidishaji vikali. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 10 ppm kama TWA, 15 ppm kama STEL; A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); (ACGIH 2004). MAK: Aina ya sarakani: 3A; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mapafu, kusababisha vidonda vya tishu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 72°C Kiwango myeyuko: -93°C Uzito wiani (maji = 1): 0.9 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 2.5 Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 11.7 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.0 |
Kiwango cha kumweka: -8°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 402°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 2.6-13.4 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 0.73 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Viwango myeyuko vinginevyo: -100°C. Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Ongezeko la kiimarishaji au kiviza huweza kuathiri tabia ya kitoksini za dutu hii, shauriana na mtaalam. Aina inayoimarisha ya hidrokwinoni ni imara kwa siku 60 tu. Kwa uhifadhi wa muda mrefu, kizuizi kingine, kama vile aminidifenili, kinashauriwa.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||