| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
Usiwashe moto. Usigusishe na asidi nitriki.
|
Poda, AFFF, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 85°C.
|
Mfumo funge wa zaidi ya 85°C, uingizaji hewa.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
|
| MFIDUO |
|
EPUKA MGUSANO WOWOTE!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuchanganyikiwa. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kukosa pumzi. Udhaifu.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Miwanivuli ya usalama.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kupumua kwa shida. (Tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Sukutua kinywa. Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. (Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu).
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T, N R: 45-23/25-36-50 S: 53-45-61 Angalia: [E] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1708-L au 61GT1-II Msimbo wa NFPA: H 3; F 2; R 0; |
Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, vyakula na malisho. Baridi. Kavu. Kilichofungwa vizuri. Uingizaji hewa kwenye sakafu.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI HADI MANJANO. HUGEUKA NYEKUNDU-KAHAWIA INAPOFIDULIWA NA HEWA NA MWANGA. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa au inapochomwa kuzalisha mafusho yenye sumu kama vile oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na vioksidishaji vikali, hasa asidi nitriki. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 2 ppm kama TWA; (ngozi); A3 (imethibitishwa kuwa kasinojeni kwa wanyama na haijulikana kama ina athari kwa wanadamu); BEI imetolewa; (ACGIH 2004). MAK: kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 2; (DFG 2004). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi na kupitia katika ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Uvukizi ifikapo 20°C ni kidogo; hata hivyo, ukolezi unaodhuru wa chembechembe zinazopeperuka hewani unaweza kufikiwa haraka wakati wa kunyunyiza. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho na ngozi. Dutu hii huweza kuathiri damu, kibofu na mafigo kusababisha vidonda vya tishu, kuharibika kwa utendaji na kufanyika kwa methemoglobini. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kuleta kuharibika kwa figo na kibofu. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri damu kusababisha kufanyika kwa methemoglobini (tazama Vidokezo). Dutu hii ina uwezekano wa kusababisha kansa kwa binadamu. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 200°C Kiwango myeyuko: -16°C Uzito wiani (maji = 1): 1.01 Umumunyifu katika maji: mbaya Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.2 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.7 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.00 Kiwango cha kumweka: 85°C c.c. Jotoridi la kujiwasha: 482°C Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.5-? Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.32 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara pendekeza. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Ona ICSC 0342, meta-Toluidine na 0343, para-Toluidine.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||