| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.
|
|
Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
|
| MLIPUKO |
|
|
|
| MFIDUO |
|
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!
|
KWA HALI YOYOTE MWONE DAKTARI!
|
| Kuvuta pumzi |
Maumivu ya tumbo. Kikohozi. Kuumwa koo. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kizunguzungu. Kusinzia. Kuchanganyikiwa. Tetemeko. Degedege.
|
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! Wekundu. Ngozi kavu. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
Wekundu. Maumivu.
|
Kingao cha uso, au au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
Maumivu ya tumbo. Kichefuchefu. Kutapika. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Kupumzika. Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Kinga ya ziada ya binafsi: nguo kamili za usalama pamoja na vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu. Uingizaji hewa. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari. Ainisho ya EU Alama: T+, N R: 26/27-51/53 S: (1/2-)-38-45-61 Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61S1702 au 61GT1-II
|
Hifadhi mahali pasipokuwa na unyevu au uchafu. Kinachotenganishwa na besi kali, metali za alkali, vyakula na malisho. Baridi. Weka gizani. Kilichofungwa vizuri. Weka katika chumba chenye uingizaji hewa mzuri.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: KIOEVU KISICHO RANGI CHENYE HARUFU TAMBULISHI. HATARI KWA MWILI: Mvuke huu ni mzito zaidi kuliko hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Dutu hii hutengana inapokanzwa na inapoathiriwa na hewa, mwanga wa urujuani iliyokoza (UV) na unyevu kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi pamoja na kloridi hidrojeni, fosjini. Humenyuka kwa ukali sana pamoja na metali za alkali, besi kali na poda ya metali nyingi kuzalisha gesi zenye sumu na babuzi. Hushambulia plastiki na mpira. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV: 1 ppm kama TWA; (ngozi); A3 (ACGIH 2005). MAK: 1 ppm, 7.0 mg/m³ Aina ya kiwango cha juu: II(2); kuingia kupitia kwa ngozi (H); Aina ya sarakani: 3B; Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2005). |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii inakera macho, ngozi na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva, ini na mafigo kusababisha kudidimiza utendaji wa mfumo mkuu wa neva na kuharibika kwa utendaji. Mfiduo huweza kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo huweza kusababisha kifo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Kioevu hukausha ngozi. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva na ini kusababisha kuharibika kwa utendaji. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 146°C Kiwango myeyuko: -44°C Uzito wiani (maji = 1): 1.59 Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 0.29 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 647 Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.8 |
Uzito wiani wa mvuke/hewa mahuluti ifikapo 20°C (hewa = 1): 1.03 Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 2.39 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii ni sumu kwa viumbe viishivyo majini.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Matumizi ya vileo huongeza athari zinazodhuru. Onyo la harufu wakati kikomo thamani cha mfiduo kinapovukwa halitoshi. Usitumie karibu na moto au uso moto, au wakati wa kulehemu.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||