PHTHALIC ANHYDRIDE ICSC: 0315
Mei 2003

1,2-Benzenedicarboxylic acid anhydride
Phthalic acid anhydride
1,3-Isobenzofurandione
CAS # 85-44-9 C8H4O3 / C6H4(CO)2O
RTECS # TI3150000 Masi ya molekuli: 148.1
UN #
EC # 607-009-00-4
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka.
Usiwashe moto.
Mnyunyizio wa maji, povu, poda kavu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.

MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI! EPUKA MGUSANO WOWOTE!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kufanyiza kisauti wakati wa kupumua.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Maumivu ya tumbo.
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 22-37/38-41-42/43
S: (2-)-23-24/25-26-37/39-46
Ainisho ya UN

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Msimbo wa NFPA: H 3; F 1; R 0;
Kinachotenganishwa na dutu zenye kuungua na za kunakisi, vioksidishaji vikali, besi kali, asidi kali, vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Uingizaji hewa kwenye sakafu. Kavu. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
PHTHALIC ANHYDRIDE ICSC: 0315
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE ING'ARAYO NYEUPE YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapogusana na maji ya moto huzalisha asidi ya ftaliki. Humenyuka ikiwa na vioksidishaji vikali, asidi kali, besi kali na kinakisishaji. Kwa kuichoma humenyuka kwa ukali pamoja na oksidi ya shaba au nitriti sodi kusababisha athari ya mlipuko. Hushambulia metali nyingi iwapo kuna maji.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 1 ppm kama TWA; SEN; A4 (haijaainishwa kama kasinojeni kwa binadamu); (ACGIH 2003).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); uhisishaji wa koromeo la hewa (Sa); (DFG 2002).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya erosoli yake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Kikolezo cha chembechembe zilizo hewani yaweza kufikiwa haraka ikitawanywa hasa kama poda.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali irritating to macho, ngozi na njia ya upumuaji.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kuhisisha ngozi. Kuvuta hewa kwa kurudia au muda mrefu huweza kusababisha pumu (ona Vidokezo).
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 284°C (usablimishaji)
Kiwango myeyuko: 131°C
Uzito wiani: 1.53 g/cm³
Umumunyifu katika maji: mmenyuko kwa polepole
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: <0.3
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 5.1
Kiwango cha kumweka: 152°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 570°C
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 1.7-10.4
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.6
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii inaweza kusafirishwa ikiwa katika hali ya kuyeyuka. Aghalabu dalili za pumu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Kwa hiyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Mtu yeyote aliyeonyesha dalili za pumu kutokana na dutu hii kamwe asigusane na dutu hiyo tena. Kwa vitu vyenye zaidi ya 0.05% ya anhidridi maleiki (maleic anhydride) namba ya UN ni 2214, daraja la 8 la hatari, kundi la III la kufungashwa na kadi ya Dharura ya kusafirishia ni TEC (R)-80S2214. Usichukue nguo za kazi nyumbani.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005