TRICHLOROMETHANESULFENYL CHLORIDE ICSC: 0311
Mei 2003

Trichloromethanesulfenyl chloride
Trichlormethyl sulfur chloride
Thiocarbonyl tetrachloride
Trichloromethyl sulfochloride
Perchloromethyl mercaptan
CAS # 594-42-3 CCl4S / CCl3SCl
RTECS # PB0370000 Masi ya molekuli: 185.9
UN # 1670
EC #
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Haiwaki. Hutoa moshi (au gesi) wenye kukereketa au wenye sumu ukiwa motoni.

Moto unapotokea katika eneo: vitenzi vyote vya kuzimia moto vinaruhusiwa.
MLIPUKO


MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kupumua kwa shida. Kichefuchefu. Kutapika. Degedege.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Mkao wa nusu wima. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu. Maumivu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho Wekundu. Maumivu.
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza Msokoto wa tumbo. (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Usimtapishe. Umpe maji mengi ya kunywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: vazi linalokinga kemikali linalojumuisha kifaa binafsi cha kupumulia.
Furushi madhubuti; weka furushi linaloweza kuvunjika katika chombo madhubuti kilichofungwa. Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: I
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61GT1-I
Kinachotenganishwa na vyakula na malisho. Tazama Hatari za Kikemikali. Kilichofungwa vizuri.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
TRICHLOROMETHANESULFENYL CHLORIDE ICSC: 0311
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU MANJANO, KAMA MAFUTA CHENYE HARUFU KALI.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapokanzwa huzalisha mafusho yenye sumu na babuzi pamoja na sulfidi hidrojeni na oksidi za sulfuri. Dutu hii hutengana inapogusana na maji huzalisha kloridi hidrojeni, dioksidi sulfuri na dioksidi kaboni. Humenyuka pamoja na besi, vioksidishaji na kinakisishaji. Hushambulia metali nyingi.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.1 ppm (ACGIH 2003).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru unaweza kufikiwa haraka sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kwa ukali macho, ngozi na njia ya upumuaji. Kuvuta pumzi wa viwango vya juu (mvuke) kunaweza kusababisha uvimbe wa mapafu (tazama Vidokezo). Mfiduo juu zaidi ya OEL huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 147-148°C
Uzito wiani (maji = 1): 1.7
Umumunyifu katika maji: hakuna
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 20°C: 0.4
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 6.4
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Madhara kwa mazingira ya mkabala na dutu hii hayajachunguzwa vya kutosha. Dalili za uvimbe wa mapafu aghalabu hazijitokezi mpaka baada ya masaa kadhaa kupita, nazo hushitadi kwa kazi za sulubu. Hivyo mapumziko na uchunguzi wa kitibabu ni muhimu. Matumizi ajilani ya matibabu ya kuvuta hewa unaotolewa na daktari au mtu aliyeidhinishwa naye yanahitajika. Jina Perchloromethyl mercaptan pia hutumika kwa ajili ya kuchanganya na CAS namba 75-70-7 (CCl_3SH).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005