3-NITROANILINE ICSC: 0307
Machi 2001

m-Nitroaniline
1-Amino-3-nitrobenzene
C.I. 37030
CAS # 99-09-2 C6H6N2O2
RTECS # BY6825000 Masi ya molekuli: 138.1
UN # 1661
EC # 612-012-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huwaka. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
Usiwashe moto. Usigusishe na vitu viwakavyo.
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
MFIDUO
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!

Kuvuta pumzi Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu.
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
Macho
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho.
Ainisho ya EU
Alama: T
R: 23/24/25-33-52/53
S: (1/2-)-28-36/37-45-61
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1
Kikundi Ufungashaji cha UN: II
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b
Msimbo wa NFPA : H3; F1; R2;
Kinachotenganishwa na asidi kali, vioksidishaji vikali, dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho. Kavu.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
3-NITROANILINE ICSC: 0307
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
FUWELE MANJANO

HATARI KWA MWILI:
Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa.

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu ya oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na asidi kali, vioksidishaji vikali na kinakisishaji kikali. Humenyuka pamoja na maunzi kikaboni kukiwepo unyevu, kusababisha athari ya moto.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV haifahamiki
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Athari zinaweza kuchelewa. Tazama Vidokezo.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Tazama Vidokezo.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko (hutengana): 306°C
Kiwango myeyuko: 114°C
Uzito wiani: 1.4 g/cm³
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.089
Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 25°C: 0.005
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.37
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pia shauriana na ICSC 0306 2-Nitroaniline na ICSC 0308 4-Nitroaniline.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005