| ||||||||||||||
| ||||||||||||||
|
||||||||||||||
| AINA ZA HATARI / MFIDUO | MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI | KINGA | HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO |
| MOTO |
Huwaka. Mimenyuko mingi yaweza kusababisha moto au kulipuka.
|
Usiwashe moto. Usigusishe na vitu vinawakavyo.
|
Poda, mnyunyizo wa maji, povu, dioksidi kaboni.
|
| MLIPUKO |
Chembechembe zilizotawanyika hufanya mchanganyiko ulipukao hewani.
|
Zuia utuaji wa vumbi; mfumo funge, vifaa vya umeme na taa visivyolipuka kwa vumbi.
|
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji. Zima moto ukiwa mahali pa usalama.
|
| MFIDUO |
|
ZUIA MTAWANYIKO WA VUMBI!
|
|
| Kuvuta pumzi |
Midomo au kucha kugeuka kuwa bluu. Ngozi kugeuka kuwa bluu. Kuumwa kichwa. Kizunguzungu. Kichefuchefu. Kuchanganyikiwa. Degedege. Kupumua kwa shida. Kupoteza fahamu.
|
Kinga kiambo ya utoaji moshi au kupumua.
|
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha iwapo imeelezwa. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Ngozi |
YAWEZA KUFYONZWA! (Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Glavu za kinga. Mavazi ya kinga.
|
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza ngozi kwa maji mengi au oga. Mpeleke kwa matibabu.
|
| Macho |
|
Kingao cha uso, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
|
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
|
| Kumeza |
(Zaidi tazama Kuvuta pumzi).
|
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini. Nawa mikono kabla ya kula.
|
Mtapishe (MTU MWENYE FAHAMU TU!). Mpeleke kwa daktari.
|
| KUSAFISHA MWAGIKO | UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO | |||||||
|
Zoa dutu iliyomwagiga katika vyombo vilivyofunikwa; endapo inafaa, loanisha kwanza ili kuzuia vumbi. Kusanya salio kwa uangalifu, Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio P3 cha chembe zenye sumu. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira.
|
Usisafirishe pamoja na vyakula au malisho. Ainisho ya EU Alama: T R: 23/24/25-33-52/53 S: (1/2-)-28-36/37-45-61 Angalia: [C] Ainisho ya UN Ainisho ya UN ya Hatari: 6.1 Kikundi Ufungashaji cha UN: II | |||||||
| HATUA ZA HARAKA | UHIFADHI | |||||||
|
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 61G12b Msimbo wa NFPA : H 3; F 1; R 2; |
Kinachotenganishwa na asidi kali, vioksidishaji vikali, dutu zenye kuungua na za kunakisi, vyakula na malisho.
| |||||||
| ||||||||
| |||
| DATA MUHIMU | |||
|
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA: FUWELE RANGI YA MACHUNGWA-MANJANO HATARI KWA MWILI: Mlipuko wa vumbi huweza kutokea iwapo katika umbo la poda au punjepunje, vikichanganywa na hewa. HATARI ZA KIKEMIKALI: Inapowaka hutengeneza mafusho yenye sumu ya oksidi za nitrojeni. Humenyuka pamoja na asidi kali, vioksidishaji vikali na kinakisishaji kikali. Humenyuka pamoja na maunzi kikaboni kukiwepo unyevu, kusababisha athari ya moto. VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS): TLV haifahamiki |
NJIA ZA MFIDUO: Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake, kupitia kwenye ngozi na kwa kumeza. HATARI ZA KUVUTA PUMZI: Hakuna ashirio linaloweza kutolewa kuhusu kima ambacho ukolezi unaodhuru hufikiwa kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI: Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika. Tazama Vidokezo. ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA: Dutu hii huweza kuathiri damu, kusababisha kufanyika kwa methemoglobini. Tazama Vidokezo. | ||
| TABIA ZA KIMAUMBILE | |||
|
Kiwango mchemko: 284°C Kiwango myeyuko: 71°C Uzito wiani: 1.44 g/cm³ Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 25°C: 0.126 Kanieneo mvuke, Pa ifikapo 20°C: 4 |
Kiwango cha kumweka: 168°C Jotoridi la kujiwasha: 521°C Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.44 | ||
| DATA YA MAZINGIRA | |||
|
Dutu hii inadhuru kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira kwa sababu hubakia kwenye mazingira.
| |||
| VIDOKEZO | |||
|
Kutegemeana na kiasi cha mfiduo, upimaji wa kitibabu wa mara kwa mara unahitajika. Matibabu mahsusi yanahitajika iwapo kuna uligaji kutokana na dutu hii; njia muafaka pamoja na maelekezo sharti yapatikane. Pia shauriana na ICSC 0307 3-Nitroaniline na ICSC 0308 4-Nitroaniline.
| |||
| MAELEZO YA ZIADA | |||
|
| |||
| |||
| © IPCS, CEC 2005 | |||