METHYL MERCAPTAN ICSC: 0299
Mei 2003

Methanethiol
Mercaptomethane
Methyl sulfhydrate
Thiomethanol
(silinda)
CAS # 74-93-1 CH3SH
RTECS # PB4375000 Masi ya molekuli: 48.1
UN # 1064
EC # 016-021-00-3
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua mno.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
Funga ugavi; kama haiwezekani na hakuna hatari kwa mazingira, acha moto uwake hadi ujizime; ama sivyo zima kwa kutumia Poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Michanganyiko ya gesi/hewa hulipuka.
Mfumo funge, uingizaji hewa, na vifaa vya umeme na taa visivyolipuka.
Utokeapo moto: poza silinda kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO
FUATA MASHARTI YA AFYA KIKAMILIFU!

Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa koo. Kizunguzungu. Kuumwa kichwa. Kichefuchefu. Kutapika. Kupoteza fahamu.
Uingizaji hewa, mtambo wa kutolea nje, au kinga ya kupumulia.
Hewa safi, mapumziko. Pumulisha yaweza kuhitajika. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi INAPOGUSANA NA KIOEVU: JAMIDI.
Glavu za kuhami baridi.
Vua nguo zilizosibikwa. Mpeleke kwa matibabu. UPATAPO JAMIDI: suuza kwa maji mengi, USIVUE nguo.
Macho Wekundu. Maumivu.
Miwanivuli ya usalama, au kinga ya macho pamoja na kinga ya kupumulia.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza


KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoka katika eneo la hatari. Shauriana na mtaalam. Uingizaji hewa. Usiruhusu kemikali hii iingie katika mazingira. Kinga ya ziada ya binafsi: vifaa vya kupumulia vilivyo toshelevu.
Kichafuzi cha maji/bahari.
Ainisho ya EU
Alama: F+, T, N
R: 12-23-50/53
S: (2-)-16-25-60-61
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 2.3
Jasara tanzu za UN: 2.1

HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC(R) - 20G2TF
Msimbo wa NFPA: H 4; F 4; R 0;
Isodhurika kwa moto. Kinachotenganishwa na vioksidishaji vikali, asidi. Baridi.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
METHYL MERCAPTAN ICSC: 0299
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
GESI ISO RANGI YENYE HARUFU TAMBULISHI.

HATARI KWA MWILI:
Gesi hii ni nzito kuliko hewa na huweza kusafiri ardhini, uwakaji wa mbali unawezekana..

HATARI ZA KIKEMIKALI:
Dutu hii hutengana inapochomwa huzalisha mafusho yenye sumu pamoja na oksidi za sulfuri na sulfidi hidrojeni. Humenyuka kwa ukali sana ikiwa na vioksidishaji vikali. Humenyuka pamoja na maji, moshi au asidi kufanya gesi inayoweza kuwaka na yenye sumu.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 0.5 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: 0.5 ppm, 1.0 mg/m³; Aina ya kiwango cha juu: II(2); Kundi la waja wazito lililo hatarini: IIc; (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru wa gesi hii hewani utafikiwa kwa haraka sana isipodhibitiwa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera macho na njia ya upumuaji. Dutu hii huweza kuathiri mfumo mkuu wa neva kusababisha kushindwa kupumua. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kupoteza fahamu. Mfiduo wa viwango vya juu huweza kusababisha kifo. Athari zinaweza kuchelewa. Uchunguzi wa kitibabu unahitajika.

TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 6°C
Kiwango myeyuko: -123°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.9
Umumunyifu katika maji, g/100 ml ifikapo 20°C: 2.3
Kanieneo mvuke, kPa ifikapo 26.1°C: 202
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 1.66
Kiwango cha kumweka: gesi iunguayo
Vikomo vya kilipukaji, % ujazo katika hewa: 3.9-21.8
DATA YA MAZINGIRA
Dutu hii ni sumu kali kwa viumbe viishivyo majini. Inashauriwa sana kutoruhusu kemikali hii iingie kwenye mazingira.
VIDOKEZO
Pindua silinda ivujayo ili mvujio uwe juu kuzuia gesi isitoke katika hali ya uoevu.
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005