2-METHYLCYCLOHEXANOL ICSC: 0294
Machi 2001

o-Methylcyclohexanol
2-Hexahydromethylphenol
o-Hexahydromethylphenol
CAS # 583-59-5 C7H14O
RTECS # GW0220000 Masi ya molekuli: 114.2
UN # 2617
EC # 603-010-00-9
AINA ZA HATARI / MFIDUO MADHARA YA PAPO HAPO / DALILI KINGA HUDUMA YA KWANZA / UZIMAJI MOTO
MOTO Huungua.
Usiwashe moto, usiwashe cheche, usivute sigara.
AFFF, povu linalokinza alkoholi, poda, dioksidi kaboni.
MLIPUKO Mvuke/hewa mahuluti inayolipuka huweza kufanyika inapovuka 58°C.
Mfumo funge wa zaidi ya 58°C, uingizaji hewa.
Utokeapo moto: poza mapipa, n.k. kwa kunyunyizia maji.
MFIDUO


Kuvuta pumzi Kikohozi. Kuumwa kichwa.
Uingizaji hewa.
Hewa safi, mapumziko. Mpeleke kwa matibabu.
Ngozi Wekundu.
Glavu za kinga.
Vua nguo zilizosibikwa. Suuza na kisha safisha ngozi kwa maji na sabuni.
Macho Wekundu.
Miwani ya usalama.
Kwanza safisha macho vizuri kwa dakika chache (ondoa lenzi mboni kama inawezekana kuziondoa kwa urahisi), kisha mpeleke kwa daktari.
Kumeza
Usile, usinywe wala kuvuta sigara ukiwa kazini.
Sukutua kinywa. Mpeleke kwa daktari.
KUSAFISHA MWAGIKO UFUNGASHAJI / UWEKAJI LEBO
Ondoa vyanzo vyote vya moto. Kusanya kioevu kinachovuja na kilichomwagika katika vyombo vilivyozibwa kadri inavyowezekana. Fyonza kioevu kilichosalia katika mchanga au kifyonzi ajizi na kisha peleka mahala pa usalama. Kinga ya ziada ya binafsi: kipumulio chujio cha gesi na mivuke ya kikaboni.
Ainisho ya EU
Alama: Xn
R: 20
S: (2-)-24/25
Angalia: [C]
Ainisho ya UN
Ainisho ya UN ya Hatari: 3
Kikundi Ufungashaji cha UN: III
HATUA ZA HARAKA UHIFADHI
Kadi ya Dharura ya Usafiri: TEC (R)-30GF1-III
Msimbo wa NFPA : H ; F 2; R 0;
Isodhurika kwa moto.
IPCS
International
Programme on
Chemical Safety
Imetayarishwa katika muktadha wa ushirikiano kati ya Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali na Tume ya Jumuiya za Ulaya © IPCS, CEC 2005

TAZAMA TAARIFA MUHIMU ILIYO NYUMA
2-METHYLCYCLOHEXANOL ICSC: 0294
DATA MUHIMU
HALI MAUMBILE; INAVYOONEKANA:
KIOEVU KISICHO RANGI, KINATACHO, CHENYE HARUFU TAMBULISHI.

VIKOMO VYA MFIDUO WA KAZI (OELS):
TLV: 50 ppm kama TWA; (ACGIH 2004).
MAK: IIb (thamani ya MAK bado haijapatikana lakini hati kamili ipo); (DFG 2004).
NJIA ZA MFIDUO:
Dutu hii huweza kufyonzwa ndani ya mwili kwa kuvuta pumzi ya mvuke wake na kwa kumeza.

HATARI ZA KUVUTA PUMZI:
Ukolezi unaodhuru hautafikiwa au utafikiwa polepole sana kutokana na uvukizi wa dutu hii ifikapo 20°C.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MFUPI:
Dutu hii inakera kidogo macho na ngozi. Mfiduo wa viwango vya juu wa mvuke huweza kuleta mkereketo wa macho na sehemu ya njia ya kuingizia hewa.

ATHARI ZA MFIDUO WA MUDA MREFU AU UNAORUDIWA:
Mgusano unaorudiwa au wa muda mrefu huweza kusababisha ugonjwa wa ngozi.
TABIA ZA KIMAUMBILE
Kiwango mchemko: 165-166°C
Kiwango myeyuko: -9.5°C
Uzito wiani (maji = 1): 0.93
Umumunyifu katika maji: mbaya
Uzitowiani wa mvuke (hewa = 1): 3.9
Kiwango cha kumweka: 58°C c.c.
Jotoridi la kujiwasha: 296°C
Oktanoli/kizigeu mgawo cha maji kwa logi Pow: 1.84
DATA YA MAZINGIRA

VIDOKEZO
Dutu hii ipo katika isoma mbili za kijiometri (cis na trans) na yaweza kuwa na umbo kinuru. Viwango myeyuko vinginevyo: 7°C (cis, dl), -4°C (trans, dl). Viwango mchemko vinginevyo: 165°C (cis, dl), 167.5°C (trans, dl).
MAELEZO YA ZIADA


TAARIFA YA KISHERIA Jumuiya za Ulaya (CEC) au Mpango wa Kimataifa kuhusu Usalama wa Kikemikali (IPCS) au mtu yeyote kwa niaba ya CEC au IPCS hatawajibika kwa matumizi ya maandishi haya.
© IPCS, CEC 2005